Maguri atua Polokwane Afrika Kusini

Mshambuliaji wa zamani wa Simba aliyekuwa akicheza soka la kulipwa nchini Oman, Elias Maguli amekamilisha uhamisho wa kujiunga na Polokwane City inayoshiriki liki kuu ya Afrika Kusini (PSL) akiwa kama mchezaji huru. Maguli amemaliza mkataba wake na klabu yake ya Dhofar FC ya Oman.

Kukamilika kwa dili hilo la kujiunga na Polokwane kunamaliza tetesi za mshambuliaji huyo kujiunga na vilabu vya Simba na Yanga ambavyo awali vilihusishwa kuwania saini yake katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili nchini. Polokwane wamekubali kiwango cha maguli kwa kumuona kwenye michuano ya COSAFA na kukubali kumsajili moja kwa moja bila kufanya majaribio.

Maguli anaungana na Abdi Banda anaekipiga na klabu ya Baroka FC ya Afrika Kusini huku wote kwa pamoja wakiwa ni wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania . kwa sasa Maguli yupo na timu ya taifa ya Tanzania bara ‘Kilimanjaro Stars’ inayoshiriki michuano ya kombe la Chalenji nchini Kenya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *