Lwandamina awaanzisha Tambwe, Chirwa, Niyonzima, Kamusoko, Msuva pamoja

Msuva akipongezwa na Chirwa baada ya kufunga bao la pili

Msuva akipongezwa na Chirwa baada ya kufunga bao la pili

Kocha mkuu wa Yanga SC, Geroge Lwandamina amewaanzisha Haruna Niyonzima, Amissi Tambwe, Obrey Chirwa na Thaban Kamusoko katika mchezo dhidimya Simb SC.

Nahodha Haruna Niyonzima aliyekua majeruhi pamoja na Amissi Tambwe wamerejea katika kikosi cha leo baada ya kupona majerahanyaliyokuwa yanawakabili.

Ikiwa ni mchezo wake wa kwanza dhidi ya watani wa jadi, Lwandamina ameweka viungo watatu kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo huo.

Kikosi kamili cha Yanga: Deo Munish; Juma Abdul, Haji Mwinyi, Andrew Vicent, Kelvin Yondani; Justine Zulu, Thaban Kamusoko, Haruna Niyonzima; Saimon Msuva, Amissi Tambwe, Obrey Chirwa.

Wachezaji wa akiba: Ally Mustafa, Hassan Kessy, Nadir Haroub, Said Juma, Juma Mahadhi, Geofrey Mwashiuya na Deus Kaseke.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *