Lukaku aitimua Chelsea nje FA Cup, Everton yatinga nusu fainali

Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea raia wa Ubelgiji Romelu Lukaku ameiongoza vyema Everton kusambaza kipigo cha mwizi kwa Chelsea katika mchezo wa robo fainali uliochezwa kwenye dimba la Goodison Park.

Klabu ya Everton ilifanikiwa kukata tiketi ya nusu fainali ambazo itachezwa kwenye dimba la Wembley baada ya kuitandika Chelsea kwa mabao 2-0, Mabao yote mawili yakifungwa na Romelu Lukaku kwenye dakika ya 78 na 82 ya mchezo.img_2078.jpeg

Katika mchezo huo, Chelsea ilipata pigo baada mshambuliaji Diego Costa kupokea kadi nyekundu baada ya kuonywa mara mbili na muamuzi wa mchezo huo Michael Oliver kwenye dakika ya 84 baada ya kumng’ata kiungo wa Everton Gareth Barry.

Dakika tatu baadae, Muamuzi wa mchezo huo alionyesha kadi nyekundu kiungo wa Everton Barry baada ya kumuonya mara mbili alipomchezea rafu Kiungo wa Chelsea Cesc Fabregas.

Kocha wa Muda wa Chelsea, Guus Hiddink amepoteza mchezo wake wa kwanza kwenye Kombe la FA akiwa kocha wa timu hiyo baada ya kushinda mechi sita zilizo pita.

Pia mshambuliaji Lukaku amefanikiwa kuifunga mabao Chelsea baada ya kushindwa kufanya hivyo katika mechi nne  zilizopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *