Liverpool v Manchester United: Mbwa na bata dhidi ya simba mwekundu

Namkumbuka sana mtu aliyecheza kwa mafanikio katika klabu ya Manchester United. Alikuwa mtu muhimu sana kwa nyakati zake ndani ya Old Trafford. Hakika Garry Neville alikuwa na kila sababu ya kulifananisha pambano hili na wanyama.

image

Mwaka 2014 wakati timu hizi zikijiandaa kukutana, Neville alisema “Ni mbwa na bata dhidi ya simba mwekundu”. Nyakati zimekwenda sana, wakati Neville akitamka maneno hayo, Manchester United ilikuwa nafasi ya tatu na Liverpool ilikuwa nafasi ya nne. Hivi sasa Manchester United ipo kaika nafasi ya sita huku Liverpool ikiwa nafasi ya saba.

Wanakutana kwenye Usiku wa Ulaya. Luois Van Gaal anatakiwa kujihukumu kwa kuwa kikosi chake kimeshindwa kufunga mabao mengi msimu huu, mabao 37 kibindoni. Hakuna namna ambayo unaweza kupata mafanikio pasipo kuwa na mshambuliaji mwenye uwezo wa kukuahidi mabao 15 na kuendelea. Itazame Chelsea, unafikiri ingekuwa na uwezo wa kufunga mabao mengi ingekuwa ilipo hivi sasa?

Siku zote mechi kubwa huwa hautarajii kuona ubora. Historia, kisasi na matukio ambayo hayana cha kuchangia kwenye mpira ndiyo huchukua nafasi. Ingawa ipo michezo mikubwa iliyowahi kufaidisha mboni za watazamaji.

Liverpool inaonekana kuwa hatari zaidi siku ya leo hasa kwenye idara ya ushambuliaji ambayo mpaka sasa imezalisha mabao 43. Mbali na Phillipe Coutinho ambaye chini ya Brendan Rodgers ndiye aliyeonekana kuwa tegemeo lakini kuna watu wenye kuifanya shughuli aliyokuwa akiifanya Coutinho.

Timu imeimarika sana chini ya Klopp, Simon Mignolet licha ya wengi kuamini amesimama vizuri kwenye milingoti mitatu lakini ameruhusu mabao kumi zaidi ya David De Gea aliyeruhusu mabao 27.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *