Liverpool kufuru

 

Wachezaji wa Spartak Moscow wakishangilia bao lao.


Wakicheza kwa kujiamini ndani ya dimba la Anifield, Liverpool FC waliweza kuandika historia mpya kisoka baada ya miaka 9 kupita !. Kwa mara ya kwanza toka msimu wa 2008-9 wameweza kufuzu hatua ya 16 bora klabu bingwa Ulaya kwa ushindi mnono wa goli 7-0.

Wakitumia mfumo wa 4-3-3 waliweza kuwapoteza kabisa uwanjani Spartak Moskwa na kuwashushia dhahama hiyo kubwa ya magoli 7-0. Dakika ya 4 tu ya mchezo Liverpool walipata penati baada ya Georgiy Dzhikiya kumsukuma Mohamedi Salah ndani ya 18 alipokuwa anaenda kufunga . Bila ajizi Phillipe Coutinho alifungua karamu ya magoli ya majogoo hao.

Roberto Firmiho kunako dakika ya 15 aliuingiza vyema mpira ndani ya 18 baada ya kuwatoka viungo wa Spartak Moscow mpira ulionaswa vizuri na Philippe Countinho na bila kusita akautia mpira kambani kwa goli zuri na kuwafanya Liverpool kuwa mbele kwa goli 2.

Muunganiko wa Sadio Mane , Mohamedi Salah na Roberto Firminho katika safu ya ushambuliaji ya Liverpool ulikuwa mwiba mkali kwa warusi hao ambao walionesha udhaifu mkubwa eneo la kiungo hali iliyofanya Liverpool kuwa na umiliki mkubwa wa mpira.

Dakika ya 19 Roberto Firminho akicheza kama False 9 wakipishana vyema na Mohamedi Salah aliweza kuipatia Liverpool goli la tatu!. Ni goli ambalo lilizidi kuwachanganya Spartak nakuonesha zaidi udhaifu wa kiungo chao na safu ya ulinzi.

Walikwenda mpumziko Liverpool wakiwa kifua mbele kwa goli 3-0!.

Dakika mbili tu baada ya kutoka mapumziko zilitosha kuendeleza ubabe wa Liverpool kwa Spartak baada ya Sadio Mane kufunga goli la nne! kwa ‘ volley ‘ nzuri iliyowafanya mashabiki wa Liverpool kulipuka kwa furaha.

Spartak baada ya goli hilo walirudi nyuma kujilinda kutoka mfumo wa 4-2-3-1 na kuingia 4-5-1 kitu kilichozidi kuwapa fursa Liverpool kutawala mchezo . Licha ya kuingia kwenye 4-5-1 bado walishindwa kuziba njia za mipira kwa majogoo hao ambao ‘ tempo’ na rithym yao ilikuwa juu kutokana na kuelewana vyema kwenye defending na attacking patterns. Dakika ya 50 Coutinho akionesha juhudi binafsi aliweza kuichambua safu ya ulinzi ya timu hiyo na kufunga goli baada ya mpira kumgonga kipa na kutinga nyavuni ( deflected ).

Sadio Mane aliwanyanyua tena mashabiki wa Liverpool kunako dakika ya 76 baada ya kupata pasi nzuri ya Sturridge na Mohamedi Salah akafunga karamu hiyo ya ushindi kunako dakika ya 86 kwa kufunga goli la saba!.

Ushindi huu umeifanya Liverpool chini ya kocha Jurgen Klopp kutinga hatua ya 16 bora tangia walivyofanya hivyo msimu wa 2008-9.

By Samuel Samuel

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *