Kipre Tchetche aumia goti

Kipre Tchetche vs Bidvest

Kipre Tchetche vs Bidvest

Mshambuliaji tegemeo wa klabu ya Azam, Kipre Tchetche  amepata majeraha ya goti.

Tchetche ambaye aliifungia Azam mabao matatu kwenye mchezo wa raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Bidvest Wits ya Afrika aliumia goti baada ya kuvutwa jezi na kuanguka.

Hata hivyo mwamuzi wa mchezo hakuona tendo hilo jambo ambalo lilipelekea kocha Stewart Hall kumfokea mshika kibendera wakati Tchetche akigaa gaa chini kwa maumivu.

Licha ya kuwa katika maumivu, Tchetche alilazimika kuendelea na pambano kutokana na Azam kuwa wamemaliza kutumia nafasi zao tatu za wachezaji wa akiba.

Akizungumza na mtandao wa Soka360, Tchetche amesema madaktari wa timu hiyo wamedai kuwa baada ya kumfanyia vipimo wamegundua hakupata hitilafu kubwa ya kumweka nje kwa muda.

Nimefanyiwa vipimo baada ya mchezo. Madaktari wameniambia si tatiz kubwa japo nahisi maumivu.

 

Tchetche amekuwa katika kiwango cha juu msimu huu tofauti na msimu uliopita baada ya kufikisha mabao 16 kwenye mashindano yote. Ana mabao tisa kwenye ligi kuu, pamoja na mabao manne kwenye Kombe la Kagame, mengine matatu kwenye kombe la Shirikisho Afrika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *