Kimenuka! Al Ahly yashindwa kutamba nyumbani

Fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Al Ahly dhidi ya Wydad Casablanca ya nchini Morocco imemalizika kwa timu zote kushindwa kutambiana.

Mchezo huo uliochezwa nchini Misri mbele ya mashabiki wa Al Ahly, umemalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1 na timu hio kuvutwa jezi nyumbani.

Bao la Al Ahly kwenye mchezo huo liliwekwa kimiani na nyota wake, Joel Joel kabla ya wageni kusawazisha kwenye kipindi cha kwanza cha mchezo huo.

Hadi timu hizo zinakwenda kwenye vyumba vya kubadilishia nguo hakukuwa na yeyote aliyeweza kumtambia mwenzake baada ya kutoshana nguvu.

Katika jitihada za kuhakikisha inajipapatua kujinasua kwenye sare hio, Al Ahly ilifanya mabadiliko kwenye dakika ya 78 kwa kumtoa Hamoudi na nafasi kuchukuliwa na Rabia.

Licha ya mabadiliko hayo lakini timu hio haikuweza kubadilisha ubao wa matokeo kwani mpaka mwamuzi anapuliza kipenga cha mwisho, sare ya bao 1-1 ndio iliyo kuwa matokeo ya mwisho.

Sare hio inakifanya kibarua kuwa kigumu kwenye mchezo wa marudiano utakaochezwa jijini Casabanca nchini Morocco.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *