Kilichowaponza Yanga leo mbele ya Mbao CCM Kirumba

Mbao ilipoiduwaza Yanga katika mchezo wa Nusu fainali

Mbao walikuwa bora kila idara leo. Ukiwaondoa Simba SC na Azam FC , hii ni timu ambayo inaingia katika historia ya kuinyanyasa Yanga katika dakika 90 na kuonekana ni timu ya kawaida ilihali ni mabingwa wa muda wote wa ligi kuu Tanzania.

Ulinzi

Safu ya ulinzi ya Yanga haikuwa mbaya sana licha ya kupwaya kidogo kwa kombinesheni ya Dante na Shaibu pale kati lakini kufa kwa kiungo cha kati kulisababisha safu hii husani njia ya kati kuonekana kushindwa kuwahimili Mbao kutokana na Pressure inayoanzia juu. Loth , Tshishimbi na Pato wote hawakuwa vyema kutengeneza defensive and offensive patterns dhidi ya Mbao .

Kiungo

Dakika 15 zilitosha kulijulisha bechi la ufundi la Yanga kuona Pato Ngonyani kapwaya dhidi ya viungo wa Mbao . Hii ilimfanya Tshishimbi kurudi chini , Loth nae kukosa pacha wa kumpokea mipira au kujenga nae mashambulizi ili Tambwe awe katika wakati mzuri wa kupokea mipira. Wote walirudi chini na kuwapa nafasi Mbao kuwa na uwezo wa kupanga mashambulizi, kuzitazama movements za Yanga tokea mbali na kuweza kujiandaa kuziba njia . Benchi la Yanga lilipaswa kuipa timu namba sita asilia kuwamudu Mbao ambao walikuwa na fighting spirit nzuri. Tshishimbi alipaswa kucheza sita , Loth hakuwa na kombinesheni nzuri na Tambwe hivyo angerudi nane kuisaidia timu kukaa na mpira na kujenga mashambulizi, kumtoa Piusi Buswita wing ya kulia kumwingiza ndani acheze na Tambwe halafu Mwashiuya angeingia kama winga wa kushoto na kulia kucheza Martin.

Ushambuliaji

Tambwe si kama alikuwa vibaya leo, ameshindwa kuipa Yanga ushindi kwa kukosa ulishwaji wa mipira mizuri toka pembeni na kati . Timu ilikosa muunganiko mzuri toka nyuma ili safu ya ushambuliaji iwe katika hali nzuri ya kushambulia. Hapa walimu wa Yanga waanze mapema kusuka safu ya ushambuliaji. Ni dhahiri kuwakosa kina Ngoma na Chirwa timu inakufa kabisa kwenye safu ya ushambuliaji . Kuna wakati mwalimu inakupasa viungo washambuliaji au mawinga wenye uwezo mzuri wa kukaa na mpira kuwaleta kati na kuwatengeneza kama second strikers .

SAMUEL SAMUEL

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *