Kikosi cha Simba kinachoanza dhidi ya Mwadui, Niyonzima, Nyoni jukwaani

Kocha Mkuu wa Simba SC, Mcameroon Joseph Omog amefanya mabadiliko machache katika kikosi kinachoanza leo dhidi ya Mwadui, huku mchezaji bora wa msimu uliopita Mohamed Hussein akianza.

Katika kikosi cha leo, Omog pia ameweza kumuanzisha mlinzi wa kati raiai wa Uganda, Juuko Murshid kuchukua nafasi ya nahodha Mwanjale, huku Erasto Nyoni na Niyonzima wakiwa jukwaani.

Kikosi kamili: GK Aishi Manula – Ally Shomari, Mohamed Hussein, Salim Mbonde, Juuko Murushid – James Kotei, Shiza Kichuya, Mzamiru Yassin, Emmanuel Okwi – Nicholaus Gyan, John Bocco.

Wachezaji wa akiba: Emmanuel Mseja, Jamal Mwambeleko, Fred Mwanjale, Jonas Mkude, Said Ndemla, Mwinyi Kazimoto, Laudit Mavugo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *