Kikosi Bora cha Ligi Kuu Tanzania Bara 2017 mzunguko wa kwanza

Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi akimtoka mchezaji wa Mbeya City kwenye mchezo wa Jana. [Picha/Mbeya]

1. Aishi Manula

Kwa misimu miwili mfululizo 2015-16 na 2016-17 amebaki kuwa golikipa bora nchini kwa uwezo wake langoni. Alimaliza msimu wa 2016-17 kama mlinda lango wa Azam FC na mwanzoni mwa msimu huu 2017-18 alijiunga na Simba SC nakuendelea nafasi kama mlinda mlango namba moja . Huyu ndio kipa namba moja wa timu ya taifa na ile ya bara Kilimanjaro Stars.

2. Salumu Kimenya

Hatajwi sana kwakuwa hayupo katika timu zenye mvuto magazetini na vyombo vingine vya habari yaani Yanga, Simba, Azam na Singida United . Mlinzi huyu wa kushoto anaekipiga na Tanzania Prisons ni mmoja wa walinzi makini nchini wanaojua kutimiza majukumu yao ya awali ya ulinzi na kusaidia mashambulizi. Ajira yake jeshi la Magereza imebaki kuwa kikwazo kwa timu za Kariakoo kumnyakua .

3. Erasto Nyoni

Huyu ni mchezaji kiraka namba moja nchini mwenye uwezo wa kucheza namba zote nyuma kasoro kipa pia kiungo cha chini. Majeruhi ya muda mrefu ya Zimbwe Jr aliyoyapata mwishoni mwa msimu wa 2016-17 yaliwafanya Simba SC kumtafuta mbadala wake na ndipo walipoweza kumyakua Erasto Nyoni toka Azam FC . Ni moja ya walinzi bora wa pembeni mwenye uwezo mzuri wa kuzuia , kupandisha timu pia kutoa msaada kwa viungo wa kati . Ndani ya uwanja hucheza kama reserved defensive midfielder.

4. Andrew Vicent

Tofauti na msimu wake wa awali 2016-17 Yanga walipomsajili toka Mtibwa Sugar , msimu huu wa 2017-18 amegeuka mchezaji tegemeo kama mlinzi wa kati akitengeneza pacha bora na Kelvin Yondani. Kuondoka kwa Vicente Bossou kumemfanya kupata mechi nyingi zinazomfanya kukomaa .

5. Yakubu Mohamedi

Moja ya walinzi bora wa kati toka Azam FC kwenye kura zangu amempiku asilimia mbili Kelvin Yondani wa Yanga SC . Ubora wake unaonekana vyema wakitengeneza pacha na Aggrey Morris au David Mwantika . Wameweza kuifanya Azam FC kuwa na alama 26 kwenye msimamo wa ligi wakishika nafasi ya pili kwa kuzidiwa idadi ya magoli ya kufunga na Simba SC .

6. Pappy Tshishimbi

Ni igizo jipya la Yanga SC msimu wa 2017-18 akitokea nchini Kongo ( DRC ). Ana uwezo mzuri kulitawala eneo lote la kati akitunza vyema mifumo ya ushambuliaji na ulinzi ya timu .

7. Shiza Ramadhani Kichuya

Kuondoka kwa Saimoni Msuva kwenye ligi ya Tanzania baada ya kujiunga na timu ya ligi kuu nchini Morocco Al Jadida, Kichuya anabaki kuwa winga na mshambuliaji makini wa pembeni. Kwa nyakati tofauti amekuwa msaada kwa timu yake ya Simba , Taifa Stars na Kilimanjaro heroes.

8. Tafadizwa Koutinyu

Kiungo wa Singida United huyu toka klabu ya Orlando Pirates nchini Afrika kusini. Anajua vyema kuichezesha timu yake ; mara nyingi amekuwa chachu ya kulinda mfumo wa kushambulia wa Hans Van Pluijm ambaye ni muumini mzuri wa patterns za Total Football. Msimu wa 2016-17 nafasi hii ilishikwa na kiungo wa Simba Mzamiru Yassin ambaye mechi 12 za msimu huu bado hazijafanikiwa kumrudisha katika kiwango cha msimu uliopita .

9. Obrey Cholla Chirwa

Ni mchezaji wa kigeni nchini anaeitendea vyema nafasi hii ya ushambuliaji wa kati akiwa na magoli sita kwenye ligi katika mechi 8 alizobahatika kupangwa. John Rafael Bocco wa Simba SC kwa washambuliaji wa kati ndio anachuana nae vyema akiwa na magoli matano.

10. Emanuel Okwi

Ni mmoja wa playmaker/second striker mwenye idadi kubwa ya magoli nchini akiwa na goli 8!. Ndio kinara wa kucheka na nyavu kwa mwaka 2017 kwa msimu huu wa ligi wa 2017-18. Okwi ni lulu ndani ya Simba SC akiwa vyema katika kupanga mashambulizi ya timu pia kushambulia kwa maana ya kufunga.

11. Eliud Ambokile

Ni zao la timu ya vijana ya Mbeya City akipanda timu kubwa msimu huu wa 2017-18. Ni kiungo na mshambuliaji mzuri wa pembeni hususani wing ya kushoto ingawa ana uwezo wa kucheza nafasi zote za mbele. Mpaka sasa ameifungia Mbeya City goli 4 na kutengeneza magoli matano (5) . Anawapiku wakongwe kwenye ligi akiwemo fundi wa wing hiyo ya kushoto kwa muda mrefu Haruna Niyonzima ambaye toka atue Simba akitokea Yanga hajawa na msimu mzuri kama ilivyo ada.

By Samuel Samuel

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *