Kamusoko alivyoimaliza Yanga, Makapu akaizika

Thaban Kamusoko akiingia uwanjani kuwavaa Simba katika pambano la watani wa Jadi. ( Picha/ Soka360 )

Thaban Kamusoko akiingia uwanjani kuwavaa Simba katika pambano la watani wa Jadi. ( Picha/ Soka360 )

Nyota wa Yanga, Thaban Kamusoko, hataweza kumaliza pambano baada ya kuumia na kutolewa nje.

Wengi tutakunaliani kuamini kuwa kukosekana kwa fundi huyo kutoka Zimbabwe kuliacha pengo kubwa kwa Yanga.

Kwa dakika zote alizokuwa dimbani Kamusoko alifanya kazi nzuri ambayo kwa kiasi kikubwa iliiwezesha Yanga kutawala pambano eneo la katikati kiasi cha wengi kuhofia Yanga wangefanya maafa kwa Simba.

Wakati Kamusoko alipokuwa uwanjani, Yanga walikuwa wakifika langoni mwa Simba kwa haraka kwa pasi za haraka, pia aliiwezesha Simba kutotulia na mpira kwa kurudi nyuma haraka kukaba.

Kipindi cha pili ambacho Kamusoko hakucheza ni dhahiri Yanga iliyumba na kuwaacha Simba wakitawala licha ya kucheza pungufu.

Ikumbukwe hata kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika ikiwa Simba walionesha kurudi mchezoni dakika chache tu baada ya Kamusoko kutoka.


Said Juma ' Makapu' akikabwa na Said Ndemla

Said Juma ‘ Makapu’ akikabwa na Said Ndemla


Madhara makubwa ya kukosekana kwa Kamusoko yaliitesa Yanga kwa kukosa mipira ya kupenyeza waliyoitumia kufika katika eneo la mwisho la Simba kwa haraka. Wakati Kamusoko alicheza juu Zaidi,  Said Juma Makapu aliyeingia kama mbadala alirudi nyuma na kuwapa nafasi viungo wa Simba kugongeana pasi zilizoipoteza Yanga.

Pia Makapu hakuwa mzuri sana kwenye kupiga pasi. Wakiwa mbele kwa bao moja na baadaye wakiwa na faida ya idadi ya kubwa ya wachezaji Yanga walimhitaji Zaidi Kamusoko au mbadala wake mwenye uwezo wa kupiga pasi za haraka haraka kwenda mbele si kuzuia.

Kiungo mkabaji, Mbuyu Twite angeweza jukumu hili la kupiga pasi ndefu ambazo zingewatia hofu viungo wa Simba kupanda mbele na kuwaacha walinzi wao kukabiliana kasi ya Obrey Chirwa na Simon Msuva.

Makapu hana sifa ya kupiga pasi hizo. Hata hivyo si haki kumbebesha mzigo wa dhambi Makapu wakati Haruna Niyonzima na Justine Zulu walikuwepo uwanjani.

Niyonzima na Zulu walifichwa kabisa na viungo wa Simba. Niyonzima ambaye ana uwezo wa kupiga pasi na kuipoza timu alishindwa kufanya jukumu hilo jambo ambalo hata yeye mwenyewe alikiri kuwa walifanya makosa ya kuwaacha Simba wamiiliki mpira.


Niyonzima


Zulu alichemka lakini angekataa vipi umeme mbele ya zile pasi nyingi za Simba? Kukosekana kwa Kamusoko kuliwaruhusu Simba kurudi kwenye mchezo wa soka la pasi nyingi ambayo ilikuwa ni kengele ya hatari kwa Yanga.

Hata alivyoingia Juma Mahadhi hakufanya lolote kwa kuwa kama ilivyo kwa Msuva na Chirwa anategemea mipira ya pasi za kupenyeza zinazompa uhuru wa eneo kubwa la kukimbia. Mpigaji wa hizo pasi hakuwepo na Niyonzima sijui alienda wapi maana pale Taifa hakuwepo.

Tisa kumi, lazima tumpongeze kocha wa Simba kwa kufanya maamuzi magumu na sahihi lakini kuumia kwa Kamusoko ilikuwa ni mtaji kwa Simba.

Kutolewa kwa kulisababisha safu ya kiungo ya Yanga kukosa pasi za haraka kuelekea katika lango la timu Simba huku Makapu  akionekana wazi kushindwa kuziba pengo la nyota anayeelekea kumaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *