Kama noma na iwe noma! Kapombe amjibu Hans Poppe bwana!

Baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Simba, Zackaria Hans Poppe kumwambia mlinzi wa timu hio, Shomari Kapombe kama anataka kucheza acheze au vinginevyo aondoke klabuni hapo, mlinzi huyo ameibuka na kumjibu mwenyekiti huyo.

Kapombe amesema kwamba Simba ilimsajili kutoka Azam akiwa katika hali ya majeruhi hivvyo mwenyekiti huyo hakupaswa kwenda mbele ya vyombo vya habari na kumtolea maneno makali kiasi hicho.

Mlinzi huyo aliongeza kuwa hana sababu ya kulazimisha kukaa nje ya uwanja ilhali ni mzima huku akisisitiza kwamba daktari wake alimshauri akae nje ya uwanja kwa muda nwingine zaidi.

Pia, Kapombe amesema kwamba si mara moja wala mbili amekua akicheza katika mazingira magumu hivyo mwenyekiti huyo hana sababu ya kuongea bila kuwa na uhakika.

“Kwani mara ngapi mimi nimekua nikicheza kwenye mazingira magumu, si angenifuata mwenyewe baada ya kwenda kuzungumza kwenye vyombo vya habari.

“Daktari wangu aliniambia nikae nje na bado nina majeraha, Simba walinisajili nikiwa na majeraha tangu nikiwa Azam,”alifafanua mlinzi huyo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Simba, Zackaria Hanspope alithibisha kuwa nyota huyo si majeruhi kwa sasa kama ambavyo taarifa zinaeleza juu ya mlinzi huyo.

Hanspope alisema kwamba vipimo huwa havidanganyi kwani vipimo vinaonesha kwamba Kapombe ameshapona isipokua uoga wake tu ndio unaomfanya kutotaka kucheza.

Mwenyekiti huyo alikwenda mbali zaidi na kusema kuwa hawawezi kumsajili mchezaji kwa fedha nyingi kisha asitumike hivyo kama anahitaji kuondoka kikosini humo hawamzuii kuondoka.

Kapombe alisajiliwa na Simba msimu huu kwa usajili huru akitokea Azam lakini hajaonekana kikosini humo tangu kuanza kwa msimu huu.

“Inategemea na yeye mwenyewe kama anataka kucheza acheze hataki aende, ni muoga tu msimamo ni yeye mwenyewe aamue kama anacheza acheze hataki aende, vipimo havidanganyi kwani vinaonesha kwamba tayari ameshapona.

“Hatuwezi kumsajili mchezaji kwa pesa nyingi halafu achezi, tumeshindwa kumvumilia, ni uoga tu,” alieleza Hanspope kwenye kituo cha redio cha efm.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *