Kakolanya kuanza mazoezi wiki ijayo

Kipa Benno Kakolanya ( Picha Soka360)

Kipa Benno Kakolanya ( Picha Soka360)

Mlinda mlango nambari tatu wa Yanga, Benno Kakolanya anatarajia kuanza mazoezi wiki ijayo.

Kakolanya aliyesajiliwa na Yanga kutoka kwenye kikosi cha Tanzania Prisons, alikuwa nje ya uwanja kwa wiki kadhaa kutokana na majeraha ya nyonga.

Awali nyota huyo alikuwa fiti kurejea dimbani lakini baada ya kuanza mazoezi alijitonesha tena hali iliyomfanya akae nje ya uwanja hadi wiki ijayo atakapoanza mazoezi.

Katika mazungumzo maalum na soka360, Kakolanya alisema kwamba anaendelea vizuri na anatarajia kuanza mazoezi wiki ijayo.

“Naendelea vizuri, natarajia kuanza mazoezi wiki ijayo” aliiambia soka360.

Urejeo wa nyota huyo unatarajia kuongeza upana wa kikosi kwenye kikosi cha Yanga kinachotarajia kushuka dimbani ijumaa hii kupambana na African Lyon.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *