Juuko Murshid apiga hat-trick

Juuko_1

Beki wa kati wa klabu ya Simba na timu ya taifa ya Uganda, Juuko Murshid amepata baraka ya watoto baada ya mkewe aitwaye Ruth kujifungua watoto watatu siku ya Jumatatu.

Watoto hao , wawili wa kike na mmoja wa kiume wamepewa majina ya Hadija, Hajara. na Murshid Jr.

Kocha wake wa timu ya taifa, Micho amempongeza kwa zawadi hio kuelekea mwaka mpya.

Juuko Murushid

Juuko akiwajibika uwanjani katika timu ya taifa Uganda.

Juuko yupo nchini Uganda na kikosi cha timu ya taifa, Uganda Cranes kinachojiandaa kwa ajili ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika yanayotarajiwa kuanza mwezi ujao tarehe 14 nchini Gabon.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *