Juuko ampoteza mwanaye

Juuko_1

Kwa mujibu wa habari kutoka Uganda, mtoto huyo wa kiume, aliyepewa jina la Murshid Jr. amefariki baada ya kuishi kwa siku tatu tangu azaliwe.

Mazishi yanatarajiwa kufanyika leo ikiwa ni siku ambayo kikosi cha timu ya taifa ya Uganda kinatarajiwa kuelekea Tunisia kupiga kambi ya maandalizi ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.

Mke wa Juko aitwaye Ruth alijifungua watoto watatu siku ya Jumatatu,wawili wakike waliosalia na mmoja wa kiume.

Soka360 inampa pole Juko  kwa msiba huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *