Joseph Kimwaga aungana na Shaaban Idd Azam!

Mshambuliaji wa Azam, Joseph Kimwaga anatarajiwa kurejea dimbani mapema mwezi Disemba baada ya kufanyiwa matibabu ya jeraha la paja lililokua likimsumbua kwa muda mrefu.

Kimwaga alipelekwa nchini Afrika Kusini kwenda kufanyiwa upasuaji wa paja lake ili kutibu jeraha hilo, daktari wa kikosi hicho Mwandandi Mwankemwa amethibitisha.

Daktari huyo amesema kwamba mara kwa mara wamekua na utaratibu wa kuwapeleka nchini Afrika Kusini wachezaji wao wanapohisi huenda wakawa na majeraha ya ndani kwa ndani.

Kimwaga anatarajiwa kurejea dimbani sanjari na mshambuliaji mwenzake, Shaaban Iddi ambae tayari ameshaanza mazoezi mepesi mepesi ya gym.

“Wanatarajiwa kurudi dimbani mwezi Disemba, tumekuana utaratibu wa kuwapeleka wachezaji wetu Afrika Kusini kwani ni nchi iliyoendelea sana kimatibabu,” alisema Mwankemwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *