Jamie Carragher amchana Mourinho

CARRAGHER ametoa maelezo ambayo mimi nimemuelewa vizuri sana kuhusu Mourinho na Guardiola.

Amesema kwamba kinachomponza sasa Mourinho na kinachombeba Guardiola ni aina yao ya soka wanalofundisha na si aina ya wachezaji walionao. Akaendelea kusema kwamba United ya sasa kwa kuangalia mchezaji mmoja mmoja ni bora kuliko City.

Akasema kwamba anaamini Mourinho akipewa City ya sasa isingekuwa inacheza soka la kuvutia na wala isingeshinda idadi ya mechi hizi. Na akaendelea kudai kwamba United ya sasa angekuwa nayo Pep Guardiola ingekuwa tishio sana. Maana akasema kwa kigezo kwamba hata kwa kuangalia mchezaji mmoja mmoja kwa kuanzia De Gea na Ederson wa Man City De Gea bado ni bora.

Na akaendelea mbele kwa kusema kwamba wakati United inamnunua Lukaku kwa ada kubwa City walimnunua Gabriel Jesus ambaye anazidiwa ada ya uhamisho na Luke Shaw ambaye anasugua bench aliyenunuliwa kwa pound milioni 30.

Akasema kabla ya msimu kuanza hakuna shabiki ambaye angeweza kukubali kuwalinganisha Sterling na Rashford ama Sane na Martial ambaye alitoka Monaco. Na pia hawapo Sawa Matic na Fernandinho.
Na hata De Bruyne na Pogba.
Bernado Silva na Mkhitaryan. Gundogan na Mata. Mangala na Bailly.

Kwahiyo anaona United ipo vizuri zaidi ya City ila tatizo ni Mourinho kaishiwa mbinu na sasa anatafuta visingizio tu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *