JKT Ruvu waipandishia Simba hasira, kumkosa kipa tegemeo

Kipa Said Kipao

Kipa Said Kipao

Msimu uliopita JKT Ruvu iliitumia Simba kama ngazi ya kutoshuka daraja kwa kuitwanga mabao 2-1 katika pambano la siku ya mwisho.

Kama vile haitoshi JKT Ruvu wakaigomea Simba kwa kulazimisha sare tasa katika mechi  hivyo licha ya kushika nafasi ya tatu kutoka mkiani wakiwa na pointi 13 maafande hao wana uwezo wa kutibua mipango ya Simba kujitanua kileleni kwa tofauti ya pointi nne.

Usajili wa timu zote Dirisha Dogo VPL

Kocha Bakari Shime amenukuliwa akisema hayupo tayari kupoteza mechi ya pili mfululizo baada ya kufungwa na Yanga mabao 3-0 wiki iliyopita.

Hofu pekee kwa Maafande ni kumkosa kipa wao tegemeo, Said Kipao ambaye anatumikia adhabu ya kufungiwa mechi tatu kufuatia kukutwa na hatia ya kumtukana mwamuzi. 

Kipao alikuwa kikwazo kikubwa kwa safu ya ushambuliaji ya Simba katika pambano la mzunguko wa kwanza lililomalizika kwa sare tasa.

Kiungo Mohamed Ibrahim

Kiungo Mohamed Ibrahim

Kwa upande wa Simba wao wataendelea kutamba na safu yao ya kiungo ambayo imekuwa chachu ya mabao msimu huu.

Viungo watatu, Yassin Muzamiru, Mohamed Ibrahim na Shiza Kichuya wanarajiwa kuendelea kuibeba Simba wakati ambao washambuliaji wa kati, Laudit Mavugo na Frederic Blagnon wakionekana kusuasua kucheka na nyavu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *