JKT Ruvu Stars yabadilishwa jina kukidhi mahitaji ya Club Licensing

Mchakato wa majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini kumiliki timu moja umefanikiwa baada ya kila jeshi kupata timu moja .

Jeshi la Kujenga Taifa ( JKT ) limeipitisha timu ya Ruvu JKT Stars kuwa ndio timu ya jeshi hilo na kuibadili jina kuitwa JKT Tanzania Sports Club . Hapo awali jeshi hilo walikuwa wamiliki wa timu mbalimbali kama vile Oljolo JKT , Mgambo JKT , Ruvu Shooting, Kanembwa na jinginezo .

Haya ni maagizo ya bodi ya ligi kwa taasisi kumiliki timu moja .

Jeshi la Polisi wamebakiwa pia na timu moja inayojulikana kama Police Tanzania ( PT ) .

JKT Tanzania SC inashiriki ligi daraja la kwanza kutafuta nafasi ya kurejea ligi kuu nchini .

Samuel Samuel

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *