Iniesta akohoa ujio wa Coutinho Barcelona

Kiungo wa klabu ya FC Barcelona ambaye hivi karibuni aliingia mkataba wa maisha na klabu yake hiyo, amekaririwa na vyombo vya habari hivi karibuni juu ya maoni yake kwa ujio wa Countinho toka Liverpool hapo Catalunya.

” ni mchezaji mzuri ambaye klabu imemsajili lakini sidhani kama anaweza kunifanya nistaafu soka mapema au kutoka Barcelona. Ujio wake ni changamoto kwangu na kwake ili kuipa mafanikio zaidi klabu yetu”

Wote Coutinho na Andres wanacheza kama viungo washambuliaji kitu ambacho kiliwafanya waandishi kumchokoza mkongwe huyo aliyezaliwa mwaka 1984 na kukuzwa kisoka katika shule ya kukuzia vipaji ya Barcelona ‘ La masia ‘ .

By Samuel Samuel

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *