Imethibitika! Okwi, Jjuuko, Niyonzima nje Kombe la Chalenji

Imethibitika bwana! Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uganda, Emmanuel Okwi na mlinzi wa timu ya taifa hilo, Jjuuko Murshid hawatakuepo kwenye kikosi cha timu hio kitakachoshiriki kwenye michuano ya Kombe la Chelenji.

Nyota hao hawatakuepo kwa sababu ya kutoa fursa kwa vijana wengine kujiandaa na michuano ya Kombe la CHAN inayoshirikisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani.

Kutokana na wachezaji hao kushiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara inawaondoa moja kwa moja kwenye kikosi cha Uganda kwenye michuano ya Kombe la CHAN mwakani.

Okwi na wachezaji wenzake wakishangilia ( Picha FUFA)

Uganda inaingia kwenye michuano ya Kombe la Chalenji itakayoanza Disemba 3, kama sehemu ya maandalizi ya mashindano ya CHAN, mwakani 2018.

Nae kiungo wa Rwanda, Haruna Niyonzima anaecheza kwenye Ligi Kuu ya Tanzania na kiungo mkabaji wa timu hio, Jean Baptiste Mugiraneza anaecheza kwenye Ligi Kuu ya Kenya hatokuepo kwenye timu ya taifa hilo baada ya Rwanda kufuzu kucheza CHAN mwakani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *