Ibrahimovic ashinda kesi ya madawa ya kuongeza nguvu

Ibrahimovic-742x417


Mshambuliaji wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic ameshinda kesi ya kukashifiwa kwa tuhuma za kutumia dawa za kuongeza nguvu.

Mahakama ya Sweden imemuamuru kocha wa mbio, Ulf Karlsson kulipa faini ya pauni 2500 kwa kutoa kauli za kumtuhumu nyota huyo wa Sweden kutumia dawa za kuongeza nguvu wakati akiwa Juventus.

Karlsson aliyekuwa kocha wa timu za mbio za Sweden kati ya mwaka 2001 na 2004 alidai mwaka jana  kuwa Ibrahimovic atakuwa alikuwa akitumia dawa za kuongeza nguvu kukuza misuli yake.

” Misuli ya Zlatan iliongezeka kwa kilo 10 ndani ya miezi 6 akiwa Juventus. Hio haiwezekani katika kipindi hicho kidogo.” Alidai Karlsson mbele ya jopo kabla ya kuongezea kuwa, ” Nafikiri alikuwa anatumia madawa. Nashawishika kuamini hivyo. ”

Mahakama imejiridhisha kuwa kauli hio japokuwa haitaji moja kwa moja kuwa Ibrahimovic anatumia dawa za kuongeza nguvu bado inaashiria kashfa kwa nyota huyo hivyo kumtoza faini Karlsson.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *