Huddersfield v Man United: United kuigeuza ngazi Huddersfield? Bashiri na Sportpesa

Manchester United ipo kwenye nafasi ya pili ikiwa imejikusanyia pointi 20 baada ya kushuka dimbani mara nane msimu huu, safu yake ya ushambuliaji ndio siraha kubwa ya maangamizi kwa wapinzani wao kwani imefanikiwa kufunga mabao 15 huku ikiruhusu mabao 5 pekee tangu kuanza kwa msimu huu.

Marcus Rashford alitolewa dakika za mwishoni dhidi ya Benfica, baada ya kufunga goli pekee lililowapa ushindi United siku ya Jumatano, Mourihno amethibitisha kuwa nyota huyo wa Uingereza yupo  fiti kwa ajili ya mechi hiyo, pia, amesema itakuwa ni vigumu kwa Erick Bailly kurejea siku ya Jumamosi na kuna mashaka pia kwa Fellaini na Pogba kuhusu mechi dhidi ya Hudderfield, Marcos Rojo na Ibrahimovic wanaendelea kuimarika taratibu.

Huddersfield watawakosa nyota wake kadhaa kama Michael Hefele, Jon Gorenc-Stankovic, Kasey Palmer na Philip Billing huku washambuliaji wake Steve Mounie na Collin Quaner watarejea kwa mara ya kwanza baada ya kutoka kwenye majeraha ya muda mrefu.

Vijana wa David Wagner waliuanza msimu wa Ligi Kuu kwa kishindo baada ya kuifunga Crystal Palace mabao 3 kwa 0, na kuifunga tena Newscastle goli moja kwa bila baada ya ushindi wa mechi hizo mbili, Terries wameshindwa kuibuka na ushindi katika mechi 6 na wataingia kwenye mechi hiyo dhidi ya United huku wakihofia kufungwa mechi ya tatu mfululizo kufuatia kupoteza mechi ya Swansea na Tottenham.

United wanarekodi nzuri dhidi ya Terries, wameshinda mechi 20 kati ya 45, sare 10 na Huddersfield wakiibuka na ushindi wa mechi 10, cha kufuraisha klabu hizi mbili hazijawahi kukutana tangu msimu wa mwaka 1971/1972.

Unaweza kubashiri mchezo huu kupitia SportiPesa kwa kubonyeza hapa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *