Hizi ndio mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara zijazo

Baada ya mapumziko ya mwezi mmoja kupisha michuano ya CECAFA Chalenji na kombe la FA, ligi kuu ya Vodacom mzunguko wa 12 inatarajiwa kuendelea Ijumaa, Disemba 29, 2017.

Ijumaa Azam FC watakuwa wenyeji wa Stand United Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam kuanzia Saa 1:00 usiku huku Jumamosi, Disemba 30 zikitarajiwa kupigwa mechi tatu.

Lipuli na Tanzania Prisons Uwanja wa Samora, Iringa kuanzia Saa 8:00 mchana, Mtibwa Sugar na Majimaji FC Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro na Ndanda FC dhidi ya Simba SC mechi zote kuanza saa 10:00 jioni.

Jumapili, Disemba 31,2017 mabingwa watetezi, Yanga SC watakuwa wageni wa Mbao FC Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza saa 10:00 jioni na Njombe Mji FC wataikaribisha Singida United kuanzia saa 8:00 mchana Uwanja wa Sabasaba, Njombe.

Mechi za kukamilisha mzunguko wa 12 zitachezwa katika sikukuu ya mwaka mpya, Januari 1,2018. Mbeya City wakiikaribisha Kagera Sugar Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya na Mwadui FC watakuwa wenyeji wa Ruvu Shooting mechi zote kuanzia saa 10:00 jioni.

Baada ya mechi hizo, Ligi Kuu itasimama tena kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar na raundi ya tatu ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) itakayochezwa kati ya Januari 5 na 7 mwakani 2018.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *