Hii sasa sifa! Manyika Jr amkalisha Aishi Manula!

 

Mlinda mlango wa Singida United amemkalisha  mlinda mlango wa Simba, Aishi Manula kwa kucheza mechi nyingi bila kuruhusu bao (clean sheets). Mechi ya jana ambayo Singida walishinda 1-0 dhidi ya Lipuli, Manyika alifikisha jumla ya michezo saba bila kufungwa katika mechi 10 za Ligi Kuu Tanzania Bara zilizopita.

Manula ambae ndie golikipa namba moja wa kikosi cha Taifa Stars, hajaruhusu bao katika mechi tano za ligi hio kati ya mechi tisa alizocheza hadi sasa. Amezidiwa ‘cleans sheets’ mbili na Mayika Jr lakini wawili hao wametofauiana katika idadi ya mechi walizocheza. Manyika tayari amecheza michezo 10 wakati Manula akiwa na mechi tisa huku leo akitarajiwa kucheza mechi yake ya 10 VPL wakati Simba itakapokuwa ikicheza dhidi ya Tanzania Prisons uwanja wa Sokoine Mbeya.

Manyika Jr taratibu anarejea kwenye ubora wake baada ya kuondoka Simba alipokuwa ‘anachoma mahindi’ kwa muda mrefu. Uwepo wa magolikipa wa kigeni Vicent Angban na Daniel Agyei kwa nyakati tofauti ulipelekea Manyika Jr kupoteza nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza pale Msimbazi.

Jana Ijumaa November 17, 2017 Manyika Jr ameandika rekodi yake ya kucheza mechi saba bila kuokota mpira ndani ya nyavu zake katika mechi 10 ambazo amesimama langoni, huku mchezo wa jana ukiwa ni wa tano mfululizo bila kufungwa. Hili si jambo dogo kwake amefikia rekodi ya golikipa wa Azam Razak Abarola ambaye hajaruhusu goli katika mechi saba za VPL katika mechi tisa alizocheza.

‘Clean sheets’ za Manyika Jr katika mechi 10 za VPL msimu huu

Stand United 0-1 Singida United, Singida United 1-0 Kagera Sugar, Ruvu Shooting 0-0 Singida United, Ndanda 0-0 Singida United, Mtibwa Sugar 0-0 Singida United, Singida United 0-0 Yanga na Singida United 1-0 Lipuli.

‘Clean sheets’ za Manula katika mechi 9 zilizopita VPL msimu huu

Simba 7-0 Ruvu Shooting, Azam 0-0 Simba, Simba 3-0 Mwadui, Simba 4-0 Njombe Mji na Mbeya City 0-1 Simba.

Baba mzazi wa golikipa huyo Manyika ambaye ni golikipa wa zamani wa Yanga na Taifa Stars alishawahi kuiambia shaffihdauda.co.tz kuwa,  kushuka kiwango kwa kijana wake wakati akiwa Simba kulichangiwa na mambo mengi ya nje ya uwanja na kutozingatia miiko ya soka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *