Haruna Niyonzima mali ya Simba, Manara athibitisha

 

Klabu ya Simba leo imethibitisha kumsajili kiungo wa zamani wa Yanga, Haruna Niyonzima kama ambavyo ilikua ikiripotiwa tangu mwezi Juni mwaka huu.

Katika mkutano na waandishi wa habari Afisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kiungo huyo wa kimataifa wa Rwanda amemaliza mkataba na Yanga.

” Niyonzima ni mchezaji halali wa Simba, ameshamaliza mkataba na klabu aliyokuwa anaitumikia. Atakuja Simba na kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda wiki ijayo.”

Niyonzima alidumu Yanga kwa miaka sita tangu alipotua nchini mwaka 2011 akitokea klabu ya APR ya nchini kwao Rwanda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *