Haras El Hodoud wasema dili la Ibrahim Hajib bado

Ibrahim Hajib
Klabu ya Haras El Hodoud inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Misri imesema bado haijafikia uamuzi wa kumsajili mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Hajib.

Hajib alifanya majaribio katika klabu hio na kuelezwa kufanya vizuri ikiwemo kufunga bao katika mojawapo ya mechi ya kirafiki.

Katika mazungumzo na mtandao wa Soka360, kocha mpya wa Haras El Hodoud, Mohamed Salah amesema bado hawajafikia uamuzi wa mwisho.

” Dirisha la usajili litafungwa tarehe 31, bado hatujaamua orodha ya mwisho ya wachezaji tutakaowasajili. ”

Haras El Hodoud iliteremka daraja msimu uliopita baada ya kudumu Ligi Kuu Misri kwa misimu 14 mfululizo.

Kwa sasa inashika nafasi ya tatu katika Kundi C la Ligi Daraja la Kwanza Misri ikiwa pointi 7 nyuma ya vinara wa kundi litakakotoa timu moja inayopanda.

Soma: Takwimu za mechi za Simba, Yanga nje ya Ligi Kuu 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *