Godin, Savic warejea kuivaa Barcelona

image

Mlinzi wa kati wa Atletico Madrid, Diego Godin na Stefan Savic wamerejea kutoka kwenye majeraha na wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Barcelona.

Urejeo wa nyota hao unaweza kuwa taarifa njema kwa kocha Diego Simeone anapokwenda kukabiriana na safu inayotajwa kuwa hatari kwa sasa duniani inayoongozwa na Messi, Suarez na Neymar.

Diego Godin amepona maumivu yake na anasema yupo fiti kwa ajili ya mchezo huo.

“Nimejitahidi kujiweka sawa haraka iwezekanavyo. Nimepona kwa asilimia mia hivyo nitakuwepo. Nina matumaini tutashinda vita”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *