Galatasaray yampa faraja Eboue

Galatasaray yaguswa na matatizo ya Emanuel Eboue. Yaamua kumpa kazi ya ukocha wa vijana wa chini ya miaka 14 ili kupata kipato cha kujikimu kutokana na hali ya kufirisika baada ya kutalakiana na mke wake wa kizungu Aurille.

Mkufunzi wa Galatasaray Fatih Terim amenukuliwa na vyombo vya habari vya Uturuki akizungumzia mpango huo wa kumuokoa Eboue kwa njia ya kumpa ajira ya ukocha.

Pia gwiji mwingine aliyepata kukipiga na Eboue katika klabu hiyo ya Galatasaray Hassan Sas ameahidi kumsaidia kifedha Eboue.

By Samuel Samuel

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *