FUFA yamtangaza Desabre Kocha Mkuu mpya Uganda

Shirikisho la Soka Uganda (FUFA) limemtangaza Sebastien Desabre raia wa Ubeligiji kuwa Kocha Mkuu wa timu ya Taifa Uganda ( The Cranes).

Jumla ya makocha 92 waliomba nafasi hiyo ya kazi wakiwemo makocha 5 wazawa wa Uganda.

Aidha Mathias Lule ambaye mi Kocha timu ya U20 Uganda ametangazwa kuwa kocha msaidizi wa Desabre.

Desabre amesema anazijua changamoto za soka la Afrika, kwani ana uzoefu wa miaka mingi hivyo kwa kushirikiana na Waganda ana imani watafanya vizuri

One Comment

  1. Lisungu vicent mwela

    December 29, 2017 at 12:09 pm

    Waganda wenzetu wako makini baada ya kuachana micho wameleta kocha mwingine wa kigeni lakini Hapa kwetu tuliambiwa Mayanga ni kocha wa muda lakini mpaka leo ni zaidi ya mwaka hatujasikia kitu kipya kutoka kwa viongozi kuhusu kocha wa kudumu wa Taifa stars hivyo kuna kitu cha kujifunza kutoka kwa majirani zetu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *