Francis Coquelin kujiunga na Valencia – Arsene Wenger

Baada ya mtanange wa ligi kuu nchini England dhidi ya Chelsea, kocha mkuu wa Arsenal Arsene Wenger amethibitisha habari za kiungo wake Francis Coquellin raia wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 26 kujiunga na klabu ya Valencia.

Msimu huu wa 2017-18 kiungo huyo amepata kucheza mechi moja tu hivyo Wenger na jopo lake la benchi la ufundi wameona si vyema kumzuia kuondoka kutokana na kukosa namba kwenye kikosi chao.

Kabla ya kufunguliwa kwa dirisha dogo la usajili Coquellin alikuwa akinyemelewa na klabu ya West Ham lakini ofa ya Valencia imemfanya Wenger kuridhia kumwachia kiungo huyo.

By Samuel Samuel

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *