Droo ya Kombe la Shirikisho (ASFC) kufanyika leo

Droo ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam (Azam Sports Federation Cup – ASFC), inatarajiwa kufanyika leo Jumatano Desemba 06, 2017 kwenye Studio za Kituo cha Televisheni cha Azam, kilichopo Tabata relini, Dar es Salaam.

Droo hiyo itasimamiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na Mdhamini wa michuano hiyo – Kituo cha Televisheni cha Azam, itachezeshwa na wachezaji wanne wa zamani.

Wachezaji hao watakaoshuhudiwa ni makipa wa zamani wa Taifa Stars ya Tanzania, Mohammed Mwameja na Steven Names kadhalika Mabeki George Masatu na Kanneth Mkapa.

Michuano hiyo ambayo Bingwa Mtetezi ni Simba SC ya Dar es Salaam, ilianza kwa kushirikisha timu 91, lakini kwa sasa zimebaki timu 64 tu ambazo zinaingia kwenye droo hiyo ya leo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *