Dondoo za tetesi za usajili Barani Ulaya

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na Arsenal, Robin Van Persie anaweza kurejea katika Ligi Kuu ya Uingereza kufuatia kuhusishwa na kutakiwa na klabu ya Crystal Palace.


Chelsea na PSG zimeingia katika vita ya kumwania beki wa Juventus, Alex Sandro ambaye anaweza kung’oka kwa bibi kizee wa Turin kwa dau la pauni milioni 61. ( Daily Mail )


Klabu ya Manchester City inaongoza mbio za kuwania saini ya mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez kufuatia kujiondoa kwa Bayern Munich inayoonekana kushindwa bei. ( Daily Mail )


Chelsea imeamua kumtupia jicho beki wa Bayern Munich, Jerome  Boateng na Kostas Manolas kujaza nafasi ya mabeki wa kati. ( Guardian )


Vilabu vya Barcelona, Manchester City na Chelsea ni miongoni mwa timu zinazowania saini ya winga wa Monaco, Thomas Leimar. (L”Equipe).


Wakala wa kiungo wa Chelsea, Mario Pasalic, wamekutana na Real Betis kujadili uhamisho wa mchezaji huyo kwenda Spain. ( Marca ).


Mshambuliaji wa Arsenal, Olivier Giroud anakaribia kurejea Ufaransa, huku Lyon na Marseille wakiripotiwa kuwa mstari wa mbele kumsajili wakati ambao Arsenal ikitajwa kuwa sokoni kusaka mbadala wake. (L’Equipe).


Arsenal imehamishia nguvu kwa Riyad Mahrez baada ya dau lake la pauni milioni 30 kwa ajili ya kuchukua Thomas Lemar kukataliwa na Monaco. ( Telegraph )

 

One Comment

  1. Mahmoud Mahmoud

    June 30, 2017 at 9:29 am

    Usajili msimu huu kadri siku zinavoenda wachezaji wanapanda bei tu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *