Dondoo za barani Ulaya leo Alhamisi

Zlatan Ibrahimovic na Paul Pogba wameanza vita ya kuwania namba ndani ya kikosi cha Manchester United kuelekea kwenye mchezo wa mwishoni mwa juma hili dhidi ya Newcastle United.

Chris Smalling, Jack Wilshere, Daniel Sturridge, Danny Welbeck na Theo Walcott hawapo kwenye mipango ya kocha wa timu ya taifa ya Uingereza, Gareth Southgate kuelekea kwenye Kombe la Dunia mwakani nchini Urusi.

Sunderland huenda ikaangukia kwa kocha wa Ireland Kaskazini, Michael O’Neill endapo Paul Heckingbottom atakataa kwenda kuifundisha timu hio.

West Brom inajiandaa kumfungashia virago kocha wake Tony Pulis kufuatia matokeo mabovu ya timu hio msimu huu.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *