Dondoo za barani Ulaya Ijumaa

Fernando Llorente amesema simu kutoka kwa kocha Maurichio Pochettino ilimshawishi kujiunga Tottenham siku ya mwisho ya dirisha la usajili. ( The Star).


Shirikisho la soka Barani Ulaya, UEFA litachunguza fujo za mashabiki zilizopelekea pambano la Europa kati ya wenyeji Arsenal na Cologne kuchelewa kuanza. ( Daily Express ).


Zlatan Ibrahimovic amewaambia mashabiki wa Manchester United watarajie mambo bab kubwa kutoka kwake pindi atakaporejea. ( Daily Express ).


Leicester City bado hawafahamu kama Shirikisho la Soka Duniani, FIFA litawaruhusu kumsajili Adrien Silva ambaye nyaraka zake za usajili zilichelewa kuwasilishwa kwa sekunde 14 siku ya mwisho ya usajili.


Nyota wa zamani wa Liverpool, Dietmar Hamann anadhani timu hio haiendi kokote chini ya kocha Jurgen Klopp. ( Liverpool Echo ).


Man city imehusishwa na Timo Werner kutoka RB Leipzig huku mchezaji mwenyewe akionekana kuvutiwa nao.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *