Conte hana habari na wanaoisema Chelsea

Antonio Conte

Kocha wa Chelsea, Antonio Conte ameikaribisha presha ya kuwa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu nchini Uingereza na kusema anafurahia kuwa katika nafasi hiyo.

Conte ambaye aliwahi kuwa kocha wa Juventus amesema pia anaamini kuwa katika nafasi hiyo siku zote kuna presha hivyo ameikaribisha huku akiamini kuendelea kufanya vizuri kwenye michezo ijayo ya Ligi hiyo.

Chelsea ipo kileleni kwa pointi 43 huku ikifuatiwa na Liverpool katika nafasi ya pili, Manchester City na Arsenal katika nafasi ya tatu na nne kimfuatano.

Kocha huyo wa Kiitalia anajivunia kuitengeza Chelsea kuwa imara kwenye eneo la ulinzi kwani mpaka sasa ndiyo timu iliyoruhusu mabao machache kuliko timu zote kwenye Ligi hiyo ikiwa imeruhusu mabao 11 pekee.

Kikosi cha Mauricio Pochettino, Spurs ndicho kinachofuatia kwa kutoruhusu mabao mengi baada ya kuruhusu mabao 12 na Manchester United ikiwa imeruhusu mabao 17.

“Ni furaha kukaa katika nafasi hii. Siamini kile watu wanachosema, cha muhimu sasa ni kuwa nyuma ya timu na kuna presha pindi unapokuwa kileleni” alisema.

Chelsea inatarajia kuikaribisha Bournemouth siku ya Boxing ikiwa ni muendelezo wa Ligi Kuu nchini Uingereza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *