CAF yataja kikosi bora Afrika, Samatta, Aubameyang waongoza mashambulizi

Africa Finest XI

Shirikisho la Soka barani Afrika, CAF limeweka hadharani kikosi bora cha wachezaji wa Afrika.

Kikosi hicho kilitangazwa jana usiku kwenye hafla ya utoaji tuzo kwa wachezaji wa Afrika waliofanya vizuri mwaka 2015.

Kikosi hicho kinaongozwa na Mchezaji Bora Barani Afrika, Pierre Aubamayeng wa Gabon na klabu ya Borussia Dortmund, akishirikiana na washambuliaji, Mbwana Samatta na Mualgeria Baghdad Bounedjah.

Viungo ni Andre Ayew (Ghana), Yaya Toure (Ivory Coast), Sadio Mane (Senegal), Yacine Brahimi (Algeria).

Walinzi ni: Serge Aurier (Ivory Coast ), Aymen Abdennour (Tunisia) na Mohamed Meftah (Algeria).

Mlinda mlango mkongwe wa klabu ya TP Mazembe na timu ya taifa ya JK Kongo, Robert Kidiaba ametajwa kulinda nyavu za kikosi hicho bora kwa bara la Afrika.

Mataifa ya Algeria na Ivory Coast yameongoza kwa kutoa wachezaji wengi huku taifa kubwa Nigeria likiwa halina mchezaji hata mmoja.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *