Bossou apeta mchujo wa kikosi cha mwisho Togo

Bossou

Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zinatarajiwa kuanza Januari 14 nchini Gabon, huku zikiwa simebaki siku kumi tu beki wa kutegemewa wa Yanga, Vincent Bossou amejumuishwa katika kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 kitakachoiwakilisha Togo katika michuano hio.

Kocha mkuu wa Togo, Claude Le Roy ametangaza kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 kitachoongozwa na mchezaji bora wa Afrika wa mwaka 2009, Emmanuel Sheyi Adebayor ambay hana timu mpaka sasa.

Makipa: Kossi Agassa (Huru), Baba Tchagouni (FC Marmande, Ufaransa), Cédric Mensah (Le Mans, Ufaransa)

Walinzi: Serge Akakpo (Trabzonspor, Uturuki), Sadate Ouro-Akoriko (Al Khaleej, Saudi Arabia), Djene Dakonam (Saint-Trond, Ubelgiji), Gafar Mamah (Dacia, Moldovia), Maklibè Kouloun (Dyto, Togo), Hakim Ouro-Sama (AS Togo Port, Togo), Vincent Bossou (Young Africans,Tanzania)

Viungo: Alaixys Romao (Olympiacos, Ugiriki), Matthieu Dossevi (Standard Liège, Ubelgiji), Floyd Ayité (Fulham, Uingereza), Henritsè Eninful (Doxa, ), Lalawele Atakora (Helsingborgs, Sweden), Prince Segbefia (Goztepe, Uturuki), Ihlas Bebou (Fortuna Dusseldorf, Ujerumani), Franco Atchou (Dyto, Togo), Serge Gakpe (Genoa, Italia)

Washambuliaji: Emmanuel Adebayor (Huru), Fo Doh Laba (Royal Club Berkane, Morocco), Komlan Agbendan  (WAFA SC, Ghana), Razak Boukari (Chateauroux, Ufaransa)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *