Bosi mfaransa wa Yanga ataja kilichomng’oa

Jerome Dufourg ( Picha ya hisani )

Jerome Dufourg ( Picha ya hisani )

Aliyekuwa mtendaji mkuu wa kampuni ya Yanga Yetu, ambayo iliingia mkataba wa miaka kumi ya kuikodisha na kutumia nembo ya  Yanga, Jerome Dufourg ameelezea sababu za kutimuliwa.

Dufourg aliyetua nchini mwezi Novemba mwaka jana amekiri kutimuliwa na Yanga Yetu lakini akashangazwa na taarifa zinazodai katimuliwa kwa sababu ya utendaji mbovu.

Akiongea na mazungumzo na mtandao wa Soka360, Dufourg amesema alikuja nchini  kuwa mtendaji mkuu wa klabu ya Yanga lakini alipofika akakutana kitu kinaitwa Yanga Yetu.

” Nilitakiwa kuwa mtendaji mkuu wa Yanga lakini nilipotua nchini nilibaini haikuwa hivyo bali nilibaini Yanga Yetu.”

” Hii ‘project’ ya Yanga Yetu ni kama haipo, hakuna kinachoendelea hivyo wamenipiga chini. ”

Dufourg amekanusha kupigwa chini kwa sababu ya utendaji usioridhisha.

” Suala la utendaji mbovu linatoka wapi wakati hakukuwa na kitu chochote? Nawezaje kushindwa kufanya kazi sehemu ambayo hakuna kazi? ”

“Nilikuwa nimeandaa wadhamini na mipango mingine , imebidi nibaki nayo. Naondoka wiki ijayo.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *