Borussia yainyuka Bayern bila huruma

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini Ujerumani ‘Bundesliga’, Bayern Munich wamepokea kichapo kikali cha mabao 3-1 kutoka Kwa Borussia Monchengladbach katika mchezo uliochezwa kwenye Dimba la Borussia-Park.

Borussia walitangulia kuziona nyavu kwenye Dakika ya 54 Kwa bao lililofungwa Na Oscar Wendt, Na wakazidi kuonyesha moto wao walipoongeza mabao mengine mawili kwa mpigo kupitia Lars Stindl Na Fabian Johnson kwenye Dakika ya 66 Na 68.

Photo: @Borussia

Photo: @Borussia

Bayern inayoongozwa Na kocha Joseph Guardiola ilipata bao la kufutia machozi kupitia Frank Ribery kwenye Dakika ya 81.

Matokeo mengine ya Bundesliga Jumamosi hii:

  1. FC Koln 0-1 Augsburg 

Hamburger SC 1-3 Mainz 05

Hertha Berlin 2-1 Bayer Leverkusen

Ingolstadt 1-1 Hoffenheim 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *