Bayern yaweka rekodi Bundesliga

Katika Dimba la Allianz Arena, Mabingwa watetezi wa Bundesliga Bayern Munich imeendeleza kusambaza vichapo msimu huu Baada ya kuinyuka FC Koln mabao 4-0.

Mabao hayo manne yaliwekwa nyavuni Na Arjen Robben, Arturo Vidal, Robert Lewandowski Pamoja Na kwaju wa penati uliopigwa Na Thomas Muller karibia na ukingoni mwa mchezo huo. 

 Kutokana Na matokeo haya, Bayern wanaweza rekodi ya Kushinda Mechi 1000 Za Ligi kuu ya Ujerumani ‘Bundesliga’.

“Maneno yangu ya kwanza ni kuwapongeza watu wote waliopo FC Bayern. Ushindi wa Mechi 1000 ni jambo kubwa sana. Na Nina furaha kubwa kuwa Kocha wa Timu Hii.” Alisema Kocha wa Bayern Pep Guardiola 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *