Bayern Munich v 1. FC Koln: Mchezo Wa Rekodi

Bayern Munich wanafukuzia rekodi ya kushinda michezo 1,000 ya Ligi Kuu nchini Ujerumani, Bundesliga leo hii watapopepetana na FC Koln.

Pep Guardiola kocha wa Bayern Munich amesema “Tukishinda maisha yanaendelea, tukifungwa maisha yanaendelea”.

Ikumbukwe mpaka sasa Bayern wamefanikiwa kushinda mara 999 katika Bundesliga ikiwa ndio timu iliyoshinda michezo mingi zaidi ya Bundesliga.

Pia kocha Pep, amesema kuwa mshambuliaji Arjen Robben yupo fiti na atakuwepo kwenye kikosi chake kwenye pambano hilo.

  
“The Bavarians” walipoteza mchezo dhidi ya Arsenal katika michuano ya Ligi ya mabingwa Ulaya, hakuna namna rahisi ambayo wanaweza kuruhusu kupoteza michezo miwili mfululizo huku mbele yao kukiwa na rekodi inayowasubiri.

Pamoja na kwamba FC Koln wamekuwa wanyonge kwa Bayern Munich lakini wanaweza kuizuia endapo wataamua kucheza mpira wa mashambulizi ya kushitukiza. Bayern Munich ni timu ambayo inamiliki mpira kwa muda mrefu na FC Koln wakiingia na akili hii, watakogeshwa mvua ya mabao.

Ratiba ya mechi za Bundesliga wikiendi hii: 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *