Barcelona yaua, Real Madrid moto, Sevilla na Valencia hawashikiki

image

Washindani wa Ballon d'Or jana hawakucheza kwenye ushindi wa timu zao.

Timu ya Barcelona imeifumua kipigo cha paka mwizi timu ya Villanovense cha mabao 6-1 kwenye mchezo wa Kombe la Mfalme.

Shukrani kwa mabao ya Dani Alves mnamo dakika ya nne ya mchezo, Sandro Ramirez aliyepiga mabao matatu(hat-trick) na bao la Munir mnamo dakika ya sabini na sita ya mchezo.

Mchezo mwengine uliwakutanisha Real Madrid dhidi ya Cadiz, mchezo uliokwisha kwa Real Madrid kuinyuka Cadiz mabao 3-1.

Mabao ya Real Madrid yamewekwa kambani na Isco aliyeweka kambani mabao mawili na Cheryshev.

Michezo mengine iliyochezwa hiyo jana ni Rayo Vallecano waliyoifunga Getafe mabao 2-0.

Real Betis waliifunga Sporting Gijon mabao 2-0.

Llagostera ilinyukwa 2-1 na Deportivo La Coruna.

Almeria ilivurumishwa mabao 3-1 na Celta de Vigo.

Sevilla waliinyuka UD Logrones mabao 3-0.

Na Barakaldo walinyukwa na Valencia mabao 3-1.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *