Barcelona yavutwa Shati na Valencia

image

La Liga.

Valencia imeilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 timu iliyopo kwenye kasi ya ajabu ndani ya Ligi kuu nchini Hispania, Barcelona.

Barcelona inayonolewa na kocha Louis Enrique Martinez ililazimika kumaliza kipindi cha kwanza bila kufungana na timu hiyo inayonolewa na kocha Gary Naville, mwanandinga wa zamani wa Manchester United.

Barcelona ilijipatia bao hilo kwenye mchezo huo, kupitia kwa nyota wake Luis Suarez mnamo dakika ya 59 ya mchezo.

Valencia walikuja juu na kufanikiwa kujipatia bao la kusawazisha mnamo dakika ya 86 ya mchezo kupitia kwa Santi Mina.

Kwenye mchezo huo, wachezaji watatu wa Valencia walilamba kadi ya njano ambao ni Daniel Parejo, Danilo na Jose Gaya huku Javier Mascherano akionyeshwa kadi ya njano kwa upande wa Barcelona.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *