Bajaj TVS King Deluxe ya 60 yatua Dar kwa Sultan Bakari

Kampuni ya michezo ya kubashiri SportPesa Tanzania imemkabidhi mshindi wa 60 wa promosheni ya SHINDA NA SPORTPESA bajaji aina ya TVS KING DELUXE mkazi wa Tandika Dar es Salaam Ndugu. Sultani Bakari (20).

Akizungumza wakati wa makabidhiano Sultani Bakari alisema “Mimi huwa ni msomaji wa magazeti kwenye kurasa za michezo ambapo nikaona matangazo ya SportPesa na hapo ndipo safari yangu ya kucheza na SportPesa ilipoanzia.”

“Kipindi mlivyozindua promosheni yenu nilikuwa nikiweka ubashiri natumiwa meseji kwamba nikituma neno SHINDA ntapata nafasi ya kuingia kwenye droo ili kujishindia bajaji aina ya TVS KING DELUXE basi baada ya hapo na mimi nikawa natuma neno SHINDA kwenda namba 15888 kila ninapoweka ubashiri wangu.”

Kupitia hii bajaji itaniinua kwa kiasi kikubwa maisha yangu kwani mimi kazi yangu ni muuza mkaa wa jumla na rejareja kwahiyo ndugu zangu watafaidika sana hasa familia yangu”

Akizungumza baada ya kukabidhi bajaji aina ya TVS KING kwa mshindi Meneja Uhusiano wa SportPesa Tanzania Bi. Sabrina Msuya alisema, tangu promosheni hii ianze tumebahatika kupata washindu wengi sana ambao ni vijana na hili ni jambo la faraja sana kwetu kwani vijana wengi kwa sasa wanakabiliwa na changamoto ya ajira.

“Kwa kushinda bajaji itawasaidia washindi hao kujiajiri ili kuendesha maisha yao na kuajiri watu wengine, Tukiwa tunaelekea ukingoni wa promosheni hii ningependa kuwasihi vihana wote wacheze na SportPesa na kushiriki kwenye promosheni hii ili waweze kubadili maisha yao

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *