Azam yamtimua Hernandez, Ongala achukua nafasi

Atta-Agyei1-1

Uongozi wa klabu ya Azam FC leo umewafukuza kazi kocha mkuu Zeben Hernandez pamoja na wasakdizi wake kufuatia mwenendo mbaya wa timu hiyo katika michezo ya Ligi Kuu ya Vodacom inayoendelea.

Kufuatia kutimuliwa kwa Hernandez, tayari Kalimangonga Ongala kocha wa Majimaji FC ameteuliwa kukinoa kikosi leo na anatarajiwa kuanza kazi katika michuano ya kombe la Mapinduzi mapema mwezi Januari 2017 kisiwani Zanzibar.

Ongala anarejea tena kukinoa kikosi cha Azam kwa mara ya tatu, kufuatia kuwahi kuwa kocha msaidizi katika vipindi wivili tofauti.

Hernandez raia wa Hispania amedumu katika kikosi hicho kwa miezi sita tangu, tangu alipoanza kazi ya kukinoa kikosi hicho cha lamba lamba.

Tangu kuwasili kwa kocha huyo na wasaidizi wake, Azam imekua matokeo mabovu tofauti na msimu uliopita, ikiruhuhusu kufungwa mabao mengi na safu yake ya ushambuliaji ikiwa butu.

Kocha huyo amekiongoza kikosi cha Azam katika michezo 17 ya ligi kuu ya Vodaco ikiwa nafasi ya 4, akishinda michezo 7, sare 6, kufungwa michezo 4, safu ya ushambuliji ikiwa imefunga mabao 22 na kuruhusu mabao 15.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *