Azam yaendeleza wimbi la sare

Azam_squad

Klabu bingwa Afrika mashariki na kati Azam Fc leo imeendeleza tena wimbi la kumaliza mchezo kwa kutoka suluhu ya bao Moja kwa moja dhidi ya majimaji ya Songea.

Azam ndio walikuwa wa kwanza kupata bao ambapo dakika ya 8 ya mchezo Yahaya Mohammed aliipatia Azam bao la kuongoza bao ambalo lilidumu hadi mapumziko na kufanya ubao kusomeka 1-0.

Kipindi cha pili kilipoanza maji maji walionekana kutawala sehemu kubwa ya kiungo na kupeleka mashambulizi ya mara kwa mara kwa Azam mpaka dakika ya 75 ya mchezo Alex Kondo aliisawazishia Majimaji nakufanya matokeo kuwa 1-1 hadi dakika tisini zinakamilika.

Hii imekuwa sare ya pili mfululizo kwa Azam FC tangu mzunguko wa pili uanze baada ya kutoka sare ya bila kufungana na African Lyon katika uwanja wa uhuru.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *