Azam wapeta tena raundi ya awali Kombe la Shirikisho

Azam_squad

Shirikisho la Soka Barani Afrika limetoa ratiba ya Kombe la Shirikisho, CAF na kuwapanga wawakilishi wa Tanzania Bara, Azam kuanzia raundi a kwanza badala ya awali.

Kama ilivyokuwa mwaka huu, Azam itasubiri mshindi wa pambano la raundi ya awali kati ya Opara United ya Botswana na Mbabane Swallows ya Swaziland.

Azam watacheza mchezo wa kwanza nyumbani katika wiki inayoangukia Machi 10-12 na marudiano ugenini Machi 17-19 mwakani.

Washindi wa raundi ya kwanza watasubiri kucheza na timu zilizotolewa katika raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa kucheza mechi mbili za mtoano kufuzu hatua ya makundi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *