Azam na Majimaji hali tete

Azam_squad

Kikosi cha Azam chini ya benchi la ufundi la Wahispania leo kitakuwa ugenini  kwenye Uwanja wa Majimaji, Ruvuma kuwakabili wenyeji Majimaji, katika mchezo wa ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara.

Azam inayokamata nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi itakuwa inapambana kubakia kwenye mbio za ubingwa baada ya kuachwa kwa pointi 12 na vinara Simba pamoja na pointi 11 na Mabingwa watetezi, Yanga.

Usajili wa timu zote Dirisha Dogo

Matokeo ya wiki iliyopita ya pande zote mbili yanaongeza ugumu wa pambano. Azam ililazimishwa sare ya bila kufungana na African Lyon huku Majimaji ikipoteza kwa bao 1-0 mbele ya wenyeji Prisons.

Majimaji wanakamata nafasi ya 14 baada ya kujikusanyia pointi 16 hivyo mchezo wa leo ni nafasi nyingine yao ya kupigania kuchukua pointi tatu ili kujiweka katika mazingira ya kusalia katika ligi.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *