Arsenal v West Brom: Wenger ataruhusu kupoteza pointi tatu?

image

Arsenal wanahitaji ushindi kuendeleza dhamira yao ya kubaki kwenye nne bora dhidi ya West Brom kwenye dimba lao la Emirates usiku wa leo.

Washika mitutu hao, wamekwenda sare kwenye michezo yao miwili ya mwisho ya Ligi Kuu England dhidi ya West Ham na Crystal Palace.

Swali lililopo ni je Arsene Wenger ataruhusu kutopata pointi tatu kwenye michezo mitatu mfululizo?

Tony Pulis, kocha wa West Brom atawakosa Alex Pritchard, Chris Brunt mwenye maumivu ya goti na James Morrison.

Wachezaji wa Arsenal waliopo fiti kuelekea mchezo huo ni: Cech, Ospina, Bellerin, Chambers, Gabriel, Gibbs, Koscielny, Mertesacker, Monreal, Arteta, Coquelin, Elneny, Flamini, Ozil, Ramsey, Rosicky, Campbell, Giroud, Sanchez, Walcott, Welbeck.

Wachezaji wa  West Bromwich Albion waliopo fiti ni:  Foster, Myhill, Rose, Chester, Dawson, Evans, Gamboa, McAuley, O’Neil, Olsson, Pocognoli, Fletcher, Gardner, McClean, McManaman, Sandro, Sessegnon, Yacob, Anichebe, Berahino, Lambert, Rondon.

Mchezo utachezeshwa na mwamuzi Jonathan Moss.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *